Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kitengo cha matangazo na vyombo vya habari kinachohusiana na Ataba Tukufu ya Alawi kimeanza operesheni ya kufunga mabango maalumu kwa mnasaba wa Idi ya Ghadir Khum, katika mfumo wa maandalizi yanayoendelea ya kuhuisha mnasaba huu wenye baraka na kuwapokea mazuwari wanaoingia katika mji wa Najaf Ashraf.
Mhandisi Ali Ismail, mkuu wa kitengo cha matangazo, alisema: “Kitengo hiki kimeanza kufunga takriban mita za mraba (1000) za picha na mabango ya matangazo, huku kazi za kukamilisha mabango mengine ya ziada yenye ukubwa wa kati ya mita za mraba (1600) hadi (2000) zikiendelea, ili kukamilisha maandalizi ya mpango maalumu wa mnasaba huu.”
Aliongeza kuwa: “Mabango haya ya matangazo yatasambazwa katika maeneo yanayozunguka uwanja mtukufu wa Alawi, kwenye milango mikuu inayoelekea Haram Tukufu, pamoja na maeneo mbalimbali ya mkoa wa Najaf Ashraf; kwa lengo la kuonyesha mji mtukufu kwa namna inayolingana na ukubwa wa mnasaba huu na mazingira yake ya kiimani.”
Hatua hizi zinafanyika katika mwendelezo wa juhudi za Ataba Tukufu ya Alawi za kuhuisha mnasaba huu wenye baraka kupitia programu za kidini, kiutamaduni na huduma zilizoratibiwa kwa pamoja, ambazo zinasaidia kuimarisha mwenendo wa Amirul-Muuminina Ali (as).
Maoni yako